WAKURUGENZI WA TAASISI NA MASHIRIKA NCHINI WAASWA KUZINGATIA SHERIA, KANUNI, NA TARATIBU.


MWANZA.

Wakurugenzi wa Taasisi na Mashirika mbali mbali nchini wanaohudhuria mafunzo ya utawala bora, wameaswa kuzingati sheria, kanuni na taratibu katika utekelezaji wa majukumu yao ili mashirika na Taasisi wanazoziongoza ziweze kufanikiwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Wakurugenzi Tanzania (IoDT) Bw. Said Kambi akisisitiza jambo wakati wa mkutano uliojadili nafasi ya mwanamke katika uongozi hasa bodi za wakurugenzi. 
Kauli hiyo imetoleawa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Wakurugenzi Tanzania Said Kambi jijini Mwanza ambapo amewataka Wakurugenzi hao kuzingatia mafunzo hayo ili kuboresha ufanisi unaozingatia utawala bora.

Aidha, amebainisha kuwa Wakurugenzi hao wanauwezo wa kufanya kazi lakini jambo la msingi linalofanywa na Taasisi ya Wakurugenzi Tanzania ni kuyaweka mafunzo katika sayansi ya mfumo na mpangilio.

Amefafanua  kuwa mafanikio ya utawala bora yanategemea mambo mawili katika utendaji wa bodi ambayo ni uwezo au ustadi na umahiri pamoja na taratibu, kanuni na mifumo.

Hata hivyo, Mafunzo hayo ya siku tano yatagawanyika katika makundi mawili ya mafunzo ya cheti kwa wakurugenzi hamsini na nane na mafunzo kwa makatibu kumi na tano wa bodi ambao ni wanasheria.



WAKURUGENZI WA TAASISI NA MASHIRIKA NCHINI WAASWA KUZINGATIA SHERIA, KANUNI, NA TARATIBU. WAKURUGENZI WA TAASISI NA MASHIRIKA NCHINI WAASWA KUZINGATIA SHERIA, KANUNI, NA TARATIBU. Reviewed by safina radio on March 06, 2018 Rating: 5

No comments

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.