ZAIDI YA WAKAZI ELFU HAMSINI WATARAJIWA KUNUFAIKA NA MRADI MKUBWA WA MAJI CHINI YA UTEKELEZAJI WA MAMLAKA YA MJI MDOGO WA NGARAMTONI.
ARUSHA.
Zaidi ya wakazi elfu hamsini wanatarajiwa kunufaika na mradi mkubwa wa kisasa wa maji unaotekelezwa katika
mamlaka ya mji mdogo Ngaramtoni katika halmashauri ya Arusha Dc mkoani Arusha.
Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake meneja wa mamlaka ya maji
katika mji mdogo wa Ngaramtoni ndugu Clyson Kimaro amesema kuwa mradi huo
unatarijiwa kugharimu takribani kiasi cha fedha shilingi,Bilioni 5.8.
Meneja Kimaro ameongeza kuwa vitongoji
vitakavyo nufaika na mradi huo ni Ngaramtoni,Seuri,vijiji vya Lengijave,pamoja
na Olkokola,ambapo mradi huo unatazamiwa kukamilika mwezi Novemba,2018.
Mamlaka ya maji katika mji mdogo wa ngaramtoni (ngauwasa) inakabiliwa na
changamoto ya upungufu mkubwa wa maji kwa kuwa miradi iliyopo ni midogo huku
mahitaji ya maji yakiwa ni takribani lita milioni saba kwa siku.
Meneja kimaro amewaambia waandishi wa habari kuwa kiasi cha maji
kinachopatikana kwa sasa kwa siku ni lita milioni mbili na laki nane wakati
ambapo kuna upungufu wa lita milioni nne na laki mbili kwa siku.
Wakati huo huo meneja wa ngauwasa hakusita kutoa wito kwa jamii
kuyatunza mazingira kwa kuvilinda vyanzo vya maji na kuacha kukata miti kwenye
maeneo ya vyanzo hivyo.
Kitendawili kikubwa
kwa mamlaka ya maji katika mji mdogo wa ngaramtoni ni kukamilika kwa mradi huo
kwa wakati kama alivyo ahidi meneja wa mradi huo; huku vitongoji vingine kama vile vya olmotonyi,na maeneo ya jirani yakisubiri
namna yatakavyo pata huduma ya maji; kwani maeneo hayo kwa sasa yanakabiliwa na
uhaba mkubwa wa maji.
ZAIDI YA WAKAZI ELFU HAMSINI WATARAJIWA KUNUFAIKA NA MRADI MKUBWA WA MAJI CHINI YA UTEKELEZAJI WA MAMLAKA YA MJI MDOGO WA NGARAMTONI.
Reviewed by safina radio
on
March 06, 2018
Rating:

No comments