CHINA YAIJIBU MAREKANI KWA KUITISHIA MAREKANI KUTOZA BIDHAA ZAKE KODI YA DOLA BILIONI 3.


Nchi ya China imeionya Marekani kuwa haiogopi vita vya kibiashara wakati huu ikitishia kutoza kodi ya zaidi ya dola bilioni 3 kwa bidhaa kutoka nchini Marekani katika kile kinachoonekana kujibu tangazo la rais Donald Trump kutoza kodi dhidi ya bidhaa kutoka China.

Image result for China.
Rais wa Marekani upande wa bendera ya China (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa China Xi Jing Ping (kulia) upande wa bendera ya Marekani.
Utawala wa Beijing umetoa orodha ya bidhaa ambazo zitalengwa na kuongezewa ushuru wa hadi kufikia asilimia 25 kuanzia kwenye matunda hadi kwa nyama ya nguruwe licha ya kuwa imeshindwa kuchukua hatua zaidi na kuonesha nia ya kuwa na mazungumzo.

Hatua za hivi karibuni zimeshuhudia masoko ya hisa yakiporomoka wakati huu Marekani, ambayo inaituhumu Uchina kwa wizi wa haki miliki pamoja na hatua nyingine ambazo sio za haki dhidi ya makampuni yake, huenda ikachochea vita ya kibiashara.

Hata hivyo  Trump hajachukua mara moja hatua za kuweka ushuru mpya, lakini ndani ya majuma mawili waziri wa biashara wa Marekani anatarajiwa kutangaza bidhaa zilizolengwa kwenye amri hiyo ya rais Trump.

CHINA YAIJIBU MAREKANI KWA KUITISHIA MAREKANI KUTOZA BIDHAA ZAKE KODI YA DOLA BILIONI 3. CHINA YAIJIBU MAREKANI KWA KUITISHIA MAREKANI KUTOZA BIDHAA ZAKE KODI YA DOLA BILIONI 3. Reviewed by safina radio on March 23, 2018 Rating: 5

No comments