RAIS MAGUFULI LEO AMEFUNGUA MKUTANO WA 11 WA BARAZA LA WAFANYABIASHARA.


Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh John Magufuli leo amefungua mkutano wa 11 wa baraza la wafanyabiashara ikulu jijini Dar-es-Salaam.


Image result for PICHA YA MAGUFULI
RAIS MAGUFULI

Akifungua mkutano huo rais Magufuli amewataka wafanyabiashara hao kujadili kwa uwazi changamoto wanazopitia ili serikali iweze kuwasaidia na kukuza uchumi wa nchi.

Amesema kuwa serikali iko tayari kusikiliza changamoto zinazowakabili wafanyabiashara ndio maana imeamua kukutana nao wakiwa na mawaziri wa wizara zote pamoja na makatibu wakuu ambao  watachukua changamoto hizo kwa  ajili ya kuzifanyia  kazi.

Kwa upande wake mwenyekiti wa baraza la wafanyabiashara hapa nchini Dr Reginald Mengi amemshukuru rais Magufuli kwa juhudi zake za kupambana na rushwa juhudi ambazo zimesaidia kuleta ushindani wa kweli katika sekta binafsi.

RAIS MAGUFULI LEO AMEFUNGUA MKUTANO WA 11 WA BARAZA LA WAFANYABIASHARA. RAIS MAGUFULI LEO AMEFUNGUA MKUTANO WA 11 WA BARAZA LA WAFANYABIASHARA. Reviewed by safina radio on March 19, 2018 Rating: 5

No comments