VIKUNDI VYA WANAWAKE NA VIJANA WILAYANI TARIME KUCHUKULIWA HATUA.


Mkuu wa wilaya ya Tarime Mkoani Mara Bw Glorias Luoga amesema kuwa serikali itavichukulia hatua za kisheria ikiwemo kufikishwa mahakamani vikundi vya wanawake na vijana ambavyo vilichukua mkopo na kushindwa kurejesha kwa wakati.

Image result for PICHA YA MKUU WA WILAYA YA TARIME GLORIAS LUOGA
Mkuu wa wilaya ya Tarime Mkoani Mara Bw Glorias Luoga
Bw Luoga ametoa kauli hivyo wilayani humo wakati akikabidhi hundi ya shilingi milioni ishirini na moja kwa vikundi 11 vya akina mama na vijana wa halmashauri ya mji wa Tarime.
Amesema kuwa fedha walizokopeshwa wanawake na vijana hao ni asilimia kumi ya mapato ya ndani ya halmashauri ya mji wa Tarime yaliyokusanywa kutoka kwenye vyanzo vyake vya ndani.
Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri hiyo Bw Hamis Nyaswi amesmema kuwa  serikali imedhamiria kuwawezesha wananchi kuwa na shughuli za kuwainua kiuchumi hivyo haina mzaha na fedha hizo.

VIKUNDI VYA WANAWAKE NA VIJANA WILAYANI TARIME KUCHUKULIWA HATUA. VIKUNDI VYA WANAWAKE NA VIJANA WILAYANI TARIME KUCHUKULIWA HATUA. Reviewed by safina radio on March 20, 2018 Rating: 5

No comments