CANADA KUTOA NDEGE ZA KIVITA NCHINI MALI
Nchi ya Canada imesema itatuma ndege kadhaa za kivita na zile za
kusafirisha mizigo pamoja na wanajeshi watakaotoa mafunzo nchini Mali katika
kipindi cha miezi 12 kusaidia operesheni inayoendelea kufanywa na walinda amani
wa umoja wa Mataifa.
Waziri wa ulinzi wa Canada, Harjit Sajjan amewaambia waandishi
wa habari kuwa kikosi hicho maalumu kitajumuisha Helkopta mbili kubwa za kivita
ambazo zinahitajika kwa sasa kwaajili ya usafirishaji pamoja na helkopta
nyingine nne za kuendesha mashambulizi na kulinda misafara ya walinda amani.
Hata hivyo tarehe rasmi ya operesheni hii ya kwanza ya Canada
barani Afrika tangu misheni yake ya nchini Rwanda na Somalia katika miaka ya
1990 pamoja na idadi kamili ya wanajeshi watakaotumwa, haijawekwa wazi.
Hakikisho hili la Canada limekuja baada ya mwaka uliopita
Serikali ya Ottawa kusema kuwa ingetuma ndege za kivita na zile za usafirishaji
kusaidia operesheni za ukanda mjini Entebbe Uganda pamoja na kuweka tayari
kikosi chake kitakachosaidia operesheni za umoja wa Mataifa kilichokuwa na
wanajeshi 200.
Waziri wa mambo ya nje wa Canada Chrystia Freeland amesema kuwa
kikosi kitakachotumwa nchini Mali kitajumuisha wanawake ili kufikia lengo la
usawa wa kijinsia kwenye operesheni za umoja wa Mataifa za kulinda amani.
CANADA KUTOA NDEGE ZA KIVITA NCHINI MALI
Reviewed by safina radio
on
March 20, 2018
Rating:
No comments