IMEBAINISHWA KUWA NGUVU YA ROHO YA UDHAIFU HUWASHAMBULIA WATU WENYE MSAADA KWENYE FAMILIA.
Imebainishwa kuwa nguvu ya roho ya udhaifu
huwashambulia watu wanaotegemewa kwenye familia ili kuharibu uchumi na mwelekeo
wa maisha yao kwa njia ya magonjwa, zinaa, ulevi, madeni, hasira na migogoro.
Huduma ya redio Safina Kesho katika ukumbi wa Maombi
uliopo Mbauda jijini Arusha kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa sita mchana imekuandalia
maombi ya maalumu ya kuharibu msingi wa
roho ya udhaifu uliojengwa ndani ya watu.
Aidha, udhaifu wa kiroho huja ndani ya mtu iwapo mtu
hana neno la Mungu la kutosha, Nguvu za Mungu, Imani timilifu juu ya neno, Yesu
Kristo ndani yake ikiwa ni pamoja na damu ya Yesu na tabia ya maombi.
Vile vile, nguvu ya roho ya udhaifu imeonekana kuwatesa
watu kwa magonjwa, madeni, ndoa kuvunjika, biashara, pamoja na kuyumba kwa uchumi
wa mtu mmoja mmoja hadi familia.
Hata hivyo kesho watu wataombewa kulingana na
mahitaji yao hivyo kila mmoja anashauriwa kuwa na imani pamoja na kujipatanisha
na Mungu kwa njia ya maombi ya toba ili Mungu awaze kuwaokoa dhidi ya matatizo hayo
yanayowakabili.
IMEBAINISHWA KUWA NGUVU YA ROHO YA UDHAIFU HUWASHAMBULIA WATU WENYE MSAADA KWENYE FAMILIA.
Reviewed by safina radio
on
March 26, 2018
Rating:
No comments