WAKUU WA SHULE ZA SEKONDARI WATAKIWA KUEPUKANA NA IMANI ZA KISHIRIKINA..


Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Bi Zainabu Talak amezitaka shule zote za msingi na sekondari mkoani humo kuwafundisha wanafunzi wao somo la dini katika shule zao ili wawe na hofu ya Mungu na kuepukana na imani potofu za kishirikiana.

Image result for kufundisha wanafunzi wao somo la dini katika shule
Wanafunzi wakijifunza.
Bi Talak ametoa maagizo hayo wakati wa ziara yake ya kikazi wilayani Kishapu mkoani humo ambapo alitembelea miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya afya na ya maji.

Amesema kuwa wananchi wengi wamekuwa hawahudhurii katika vituo vya afya vya matibabu kwa sababu ya kuamini imani potofu hivyo kuanzia sasa shule zote za msingi na sekondari ni lazima pawepo na somo la dini ili wanafunzi hao wawe na hofu ya Mungu.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya hiyo Nyamaganga Taraba amewataka wananchi wa wilaya hiyo kuhudhuria katika vituo vya afya pindi wanapokumbwa na magonjwa badala ya kwenda kwa waganga wa kienyeji kwani nyakati hizi ni za sayansi na tekinolojia.




WAKUU WA SHULE ZA SEKONDARI WATAKIWA KUEPUKANA NA IMANI ZA KISHIRIKINA.. WAKUU WA SHULE ZA SEKONDARI WATAKIWA KUEPUKANA NA IMANI ZA KISHIRIKINA.. Reviewed by safina radio on March 16, 2018 Rating: 5

No comments