GAMBO APATA WASAA WA KUSIKILIZA CHANGAMOTO MBALI MBALI ZINAZOKABILI VIWANDA, ARUSHA.


Mkuu wa mkoa wa Arusha Bw. Mrisho Gambo  ameanza ziara ya siku tatu ya kutembelea baadhi ya viwanda vipya  na kujionea changamoto zinazo kabili viwanda hivyo  ambavyo vinatarajiwa  kuaza kazi ya uzalishaji wa bidhaa mbalimbali na kufikia malengo ya serikali ya kuwa na uchumi wa kati.

Image result for Mkuu wa mkoa wa Arusha Bw. Mrisho Gambo

Akizungumza kwenye moja ya kiwanda kipya cha kuzalisha spea za pikipiki kilichopo eneo la Themi halmashauri ya jiji la Arusha, Bw. Gambo alipata furusa ya kusikiliza changamoto mbalimbali zinazokabili kiwanda hicho na kuzitolea ufafanuzi.

Katika ziara hiyo pia Bw. Gambo ametembelea kiwanda cha kuzalisha mifuko cha kampuni ya Mornaban ambapo mkurugenzi wa fedha wa kampuni hiyo Nathan Mollel amesema kuwa kiwanda hicho kitagharimu zaidi ya shilingi bilioni tisa hadi kukamilika kwake pamoja na changamoto zinazowakabilia.

Hata hivyo, ziara hiyo ya mkuu wa mkoa wa Arusha ya  ukaguzi wa viwanda  vipya, imekuja  baada ya Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli ya kuwataka wakuu wa mikoa yote nchini kuhakikisha kila mkoa unakuwa na viwanda 100 mpaka ifikapo mwisho wa mwaka huu.


GAMBO APATA WASAA WA KUSIKILIZA CHANGAMOTO MBALI MBALI ZINAZOKABILI VIWANDA, ARUSHA. GAMBO APATA WASAA WA KUSIKILIZA CHANGAMOTO MBALI MBALI ZINAZOKABILI VIWANDA, ARUSHA. Reviewed by safina radio on March 22, 2018 Rating: 5

No comments