IGP SAIMON SIRRO AWATAKA WAKANDARASI WANAOJENGA MIRADI YA JESHI HILO MKOANI DODOMA KUMALIZA KWA WAKATI.
Mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Saimon Sirro amewataka
wakandarasi wanaojenga miradi ya jeshi hilo mkoani Dodoma kumaliza kazi hiyo
kwa wakati ili kuwezasha azma ya serikali kuhamia Dodoma.
IGP Saimon Sirro |
IGP Sirro ameyasema hayo mkoani Dodoma wakati
akikagua baadhi ya miradi ikiwemo nyumba thelathini za askari pamoja na jengo la
makazi yake kwa kupitia mradi wa unaotekelezwa kwa kutumia wataalamu wa jeshi
hilo.
Aidha, amebainisha kuwa katika ujenzi wa mradi huo
unaoendela kujengwa na wataalaumu wa ndani wa jeshi hilo hadi sasa wametumia robo
ya fedha za zilizotengwa huku akiwapongeza wakandarasi hao.
Amesema kuwa jambo la msingi ni wakandarasi hao ni kuendana
na muda ili kufanikisha mradi huo kwa haraka kwa ajili ya kuimarisha usalama
mkoani Dodoma kutokana na ongezeko la Watu katika Makao makuu ya nchi.
Hata hivyo, amewataka vijana waliopata ajira katika
mradi huo kuwa wazalendo pamoja na kutokujihusisha na vitendo vya kihalifu katika
kulinda vifaa vya ujenzi.
IGP SAIMON SIRRO AWATAKA WAKANDARASI WANAOJENGA MIRADI YA JESHI HILO MKOANI DODOMA KUMALIZA KWA WAKATI.
Reviewed by safina radio
on
March 16, 2018
Rating:
No comments