SERIKALI ZANZIBAR ITAENDELEA KUWASAIDIA WAWEKEZAJI WA NDANI.
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema kuwa
itaendelea kuwasaidia wawekezaji wa ndani ili waweze kuzalisha zaidi na kwenda
sambamba na malengo ya serikali kufikia uchumi wa kati kupitia uchumi wa
viwanda.
Kwanda. |
Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Biashara na
Viwanda Zanzibar Hassan Hamis baada ya Kamati ya Biashara, Fedha na Kilimo kutembelea baadhi ya
viwanda ikiwemo cha mifuko ya makaratasi na mjasiriamali wa kiwanda cha kufuga
ng’ombe cha Mchui ambapo amesema kuwa serikali imejidhatiti kufufua viwanda ili
kukuza uchumi wa nchi.
Mh Hamis amewataka wawekezaji wanaotaka kuanzisha
viwanda hivyo waweze kushirikiana na serikali ili kukamilisha uwekezaji huo kwa
ajili ya kuhakikisha kuwa azma na lengo la serikali ya Zanzibar ya Viwanda inatekelezeka
kwa kasi inayohitajika.
Hata hivyo baadhi ya viongozi wa kamati ya Fedha,
Biashara na Kilimo ya Baraza la Wawakilishi ikiongozwa na Kaimu Mwenyekiti Hamad
Abdala Rashidi wameishauri serikali kuweka tozo kubwa kwa biashara zinazotoka
nje.
SERIKALI ZANZIBAR ITAENDELEA KUWASAIDIA WAWEKEZAJI WA NDANI.
Reviewed by safina radio
on
March 26, 2018
Rating:
No comments