DOKTA AHMED ATEULIWA KUCHUKUA NAFASI DESALEGN NCHINI ETHIOPIA.
Mkutano wa wa viongozi wa muungano tawala wa Ethiopian People's
Revolutionary Democratic Front (EPRDF), umemteua Dokta Abiy Ahmed kuwa
mwenyekiti wa Muungano huo.
![]() |
DOKTA AHMED |
Dokta Ahmed, anayetoka jamii ya
Oromo yenye watu wengi Ethiopia, amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa muungano
unaotawala EPRDF, hatua itakayomfanya kuwa Waziri Mkuu mpya wa nchi hiyo.
Ahmed alichaguliwa kwa
zaidi ya asilimia 60 ya kura zilizopigwa kwa mujibu wa vyombo vya habari vya
serikali na atachukua wadhifa huo kutoka kwa Hailemariam Desalegn aliyetangaza
ghafla kujiuzulu mwezi uliopita.
Taifa hilo kwa sasa
liko katika hali ya dharura iliyotangazwa kwa ajili ya kumaliza maandamano ya
takriban miaka mitatu dhidi ya serikali.
Hata hivyo wakosoaji
wake wanasema ni mtu wa ndani katika
chama na hivyo hakuna matumaini kwamba
matakwa ambayo yamekuwa yakiitishwa na waandamanaji kuwa yatatekelezwa.
DOKTA AHMED ATEULIWA KUCHUKUA NAFASI DESALEGN NCHINI ETHIOPIA.
Reviewed by safina radio
on
March 28, 2018
Rating:
No comments