TRA YAANZISHA MFUMO WA PAMOJA.
Mamlaka ya Mapato Nchini TRA imeanzisha mfumo wa
pamoja unaolenga kuondoa changamoto zilizopo katika sekta ya biashara zikiwemo
ucheleweshaji wa bidhaa bandarini.
KAMISHINA MKUU TRA CHARLES KICHERE |
Hayo yamebainika katika kongamano lililokutanisha
wakuu wa taasisi za serikali na sekta binafsi utakao lenga kuondoa vikwazo
katika taasisi hizo na kuboresha mazingira ya kibiashara.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Nchini TRA Bw Charles
Kichere amesema kuwa mradi wa mfumo wa pamoja utaongeza na kurahisisha utozaji
wa tozo na katika sekta binafsi utapunguza gharama za upakuaji wa bidhaa
forodhani.
Hata hivyo Mradi huo unatajwa kuwa hatua muhimu kwa
serikali kushirikiana na taasisi mbali mbali pamoja na kuleta ufanisi kwa watu
wanaopelekewa huduma ambapo mfumo huo utalenga maeneo muhimu ikiwemo usimamizi
wa mapato, utekelezaji wa sera za biashara, usalama wa uwekezaji na ugawaji wa
bidhaa pamoja na uchukuzi bandarini na viwanja vya ndege.
TRA YAANZISHA MFUMO WA PAMOJA.
Reviewed by safina radio
on
March 29, 2018
Rating:
No comments