MZOZO WA SYRIA WAINGIA MWAKA WA NANE.


Mzozo wa Syria umeingia mwaka wa nane leo huku Uturuki ikilizingira eneo la Wakurdi upande wa Kaskazini hhuku vikosi vya serikali vikiyashambulia maeneo ya waasi karibu na mji mkuu Damascus.


Image result for PICHA ZA MAENEO YALIYOATHIRIKA NA VITA NCHINI SYRIA


Katika mapigano ya hivi karibuni vikosi vinavyoungwa mkono na Uturuki vimefanya mashambulio ya mabomu katika mji wa Afrin na kukaribia kuuzingira mji huo, katika uvamizi ambao huenda ukaibadili ramani ya kaskazini mwa Syria.

Jeshi Syria leo limethibitisha kuingia katika eneo la Ghouta Mashariki ambapo Urusi imesema imerefusha usitishaji mapigano kwa siku mbili katika mji wa Douma kwenye eneo hilo ili kuruhusu misaada ya kibinadamu.

Hata hivyo mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya mzozo wa Syria Staffan de Mistura anatarajiwa kulihutubia baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu mzozo huo.

MZOZO WA SYRIA WAINGIA MWAKA WA NANE. MZOZO WA SYRIA WAINGIA MWAKA WA NANE. Reviewed by safina radio on March 15, 2018 Rating: 5

No comments