RAIS MAGUFULI AMEWATAKA WATENDAJI WA SERIKALI KUSHIRIKIANA NA WAWEKEZAJI.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli amewataka watendaji wa serikali wakiwemo mawaziri na wakuu wa mikoa kuhakikisha wanashirikiana na wawekezaji ili kuimarisha uchumi kupitia viwanda vya ndani.


Image result for PICHA YA MAGUFULI
RAIS MAGUFULI.


Mh Magufuli ametoa maagizo hayo leo mkoani Morogoro wakati akizindua kiwanda cha Philips Moris International kinacho endeshwa na Kampuni ya Mansur Industries mkoani humo na kuwataka watanzania kuthamini bidhaa za ndani ili kukuza uchumi wa nchi.

Aidha, Rais Magufuli amewataka watanzania kubadili dhana ya kufikiria kuwa Tanzania ni soko la kuuza malighafi za nje ya nchi bali mtazamo wao uwe katika kujenga viwanda ndani ya nchi ili kufanya mabadiliko ya mapinduzi ya kiuchumi.

Hata hivyo, ameahidi kushughulikia  uwepo wa kero za kodi na ushuru mwingi unaotozwa kwa bidhaa zinazozalishwa na viwandwa vya ndani pamoja na uingizwaji wa bidhaa nyingi kutoka nje ya nchi ili kulinda uwekezaji kupitia viwanda vya ndani sambamba na kuimarisha ushindani wa soko la ndani.

Kwa upande wake waziri wa viwanda na uwekezaji nchini Mh Charles Mwijage amemuomba rais Magufuli kutembelea viwanda vilivyokamilika,huku mkuu wa mkoa wa Morogoro Dr Kebwe Stephen Kebwe akisema kuwa mkoa huo umepiga hatua katika uchumi wa viwanda.

RAIS MAGUFULI AMEWATAKA WATENDAJI WA SERIKALI KUSHIRIKIANA NA WAWEKEZAJI. RAIS MAGUFULI AMEWATAKA WATENDAJI WA SERIKALI KUSHIRIKIANA NA WAWEKEZAJI. Reviewed by safina radio on March 15, 2018 Rating: 5

No comments