JESHI LA POLISI LIMESEMA LIMEJIPANGA KIKAMILIFU KKUIMARISHA ULINZI KATIKA KIPINDI HIKI CHA PASAKA
Jeshi la Polisi Nchini limewahakikishia wananchi
kuwa limejipanga kikamilifu kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na
usalama katika kuimarisha ulinzi na usalama katika kipindi cha siku kuu ya pasaka.
IGP SIRRO |
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari Inspekta
Jenerali wa polisi IGP Saimon Sirro amesema kuwa askari wa jeshi hilo wamejipanga
vizuri ili kudhibiti vitendo vya kihalifu visifanyike na vitakapojitokeza
vitadhibitiwa kwa haraka.
Aidha, Kamanda Sirro amewataka wamiliki wa kumbi za
starehe kufuata sheria kanuni na taratibu za uendeshaji wa kumbi hizo ikiwemo
kutoruhusu Disko Toto, na kujaza watu kupita kiasi huku wazazi wakitakiwa
kuwaangalia watoto wao na kutokuwaacha wenyewe bila uangalizi.
JESHI LA POLISI LIMESEMA LIMEJIPANGA KIKAMILIFU KKUIMARISHA ULINZI KATIKA KIPINDI HIKI CHA PASAKA
Reviewed by safina radio
on
March 28, 2018
Rating:
No comments