SERIKALI DRC YAKATAA MSAADA WA EU KUTOKANA NA UMOJA HUO KUONGEZA CHUMVI KATIKA MASUALA YA KIBINADAMU.
Umoja wa Ulaya umesema unaguswa na nchi ya Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo baada ya nchi hiyo kutangaza kuwa itakataa kupokea kiasi
cha dola za Marekani bilioni 1 na laki 7 ambazo ni msaada wa kimataifa.
Bendera za Umoja wa Ulaya zikipepea katika Ofisi za Makao Makuu ya huo mjini Brussels. |
Mvutano wa maneno umeibuka kati ya umoja wa Mataifa na Serikali
ya DRC baada ya utawala wa Kinshasa Ijumaa ya wiki iliyopita kusema
haitashiriki mkutano wa kimataifa wa kuisaidia nchi hiyo fedha za misaada ya
kibinadamu mjini Geneva, Uswis, Serikali ikisema tatizo la kibinadamu
limeongezwa chumvi kuliko hali halisi.
Umoja wa Ulaya unaguswa na kuzorota kwa hali ya kibinadamu
nchini DRC, amesema mkuu wa masuala ya kibinadamu kutoka umoja wa Ulaya
Christos Stylianides wakati akizungumza na wanahabari kwenye mji wa Goma.
Waziri mkuu wa DRC Jose Makila alinukuliwa siku ya Ijumaa ya
wiki iliyopita akisema umoja wa Mataifa umoengeza chumvi na kwamba mashirika
yake ya misaada na asasi za kiraia zimekuwa zikifanya propaganda ya kuichafua
nchi yake.
SERIKALI DRC YAKATAA MSAADA WA EU KUTOKANA NA UMOJA HUO KUONGEZA CHUMVI KATIKA MASUALA YA KIBINADAMU.
Reviewed by safina radio
on
March 26, 2018
Rating:
No comments