RAIS MAGUFULI AMWAGIZA WAZIRI WA TAMISEMI KUWASIMAMISHA KAZI WAKURUGENZI WAWILI
Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh John
Magufuli amemwagiza waziri wa nchi ofisi ya rais TAMISEMI Mh Suleman Jaffo
kuwasimamisha kazi wakurugenzi wa halmashauri za wilaya ya Ujiji mkoani Kigoma
na Pangani mkoani Tanga kufuatia matumizi mabaya ya fedha za serikali.
RAIS MAGUFULI. |
Mh Magufuli ametoa maagizo hayo leo ikulu jijini
Dar-es-salaam baada ya kupokea ripoti ya fedha ya mkaguzi mkuu wa hesabu za
serikali CAG Professa Juma Mussa Hassad,ambapo amesema kuwa serikali itaendelea
kuwachukulia hatua zaidi viongozi wanaoshindwa kusimamia matumizi mazuri ya
fedha za umma.
Amesema kuwa katika ripoti hiyo ya CAG Halmashauri
hizo zilipata hati chafu hivyo ni lazima wakurugenzi hao wakae pembeni ili
kupisha uchunguzi huku akimtaka waziri mkuu Mh Kassimu Majaliwa kushirikiana na
mawaziri kupitia ripoti hiyo ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa.
Kwa upande wake waziri mkuu Mh Kasimu Majaliwa
ameahidi kuifanyia kazi ripoti hiyo ili mapungufu yaliyojitokeza yasijitokeze
tena wakati mwingine.
Akisoma ripoti hiyo mkaguzi mkuu wa hesabu za
serikali CAG Professa Juma Mussa Hassad amesema kuwa katika ukaguzi wao
wamebaini kuwa mashirika ya umma na serikali za mitaa zimefanya vizuri tofauti
na hapo awali hali inayoonyesha kuwa fedha za umma zinatumika vizuri.
RAIS MAGUFULI AMWAGIZA WAZIRI WA TAMISEMI KUWASIMAMISHA KAZI WAKURUGENZI WAWILI
Reviewed by safina radio
on
March 27, 2018
Rating:
No comments