KINARA WA UPINZANI NCHINI SIERRA LEONE AMTUHUMU RAIS ANAYEMALIZA MUDA WAKE.
Kinara wa upinzani nchini Sierra Leone Julius Maada Bio
amemtuhumu rais anayemaliza muda wake Ernest Bai Koroma kwa kujaribu
kuchelewesha kwa makusudi uchaguzi wa duru ya pili uliopangwa kufanyika Jumanne
ya wiki hii kwa kwenda mahakamani kujaribu kukifanya chama tawala kibaki
madarakani.
KINARA WA UPINZA MAADA BIO |
Mahakama kuu ya nchi hiyo mwishoni mwa juma iliiagiza tume ya
taifa ya uchaguzi kusitisha maandalizi ya kura hiyo hadi pale kesi ya
malalamiko ya uchaguzi itakaposikilizwa, kesi ambayo iliwasilishwa na mawakili
wenye uhusiano na chama tawala.
Bio ambaye alishinda duru ya kwanza katika uchaguzi wa Machi 7
kupitia chama cha Sierra Leone People's, atashindana na Samura Kamara ambaye ni
mgombea anayeungwa mkono na rais Koroma na anawakilisha chama tawala cha All
People's Congress.
Bio amesema Koroma atalazimika kuwajibika kwa chochote
kitakachotokea baadae, kuchelewa au kufutwa kwa uchaguzi kunakotengeneza hofu
ya kusababisha machafuko nchini humo.
Chama tawala cha APC kinategemea wapiga kura wa kaskazini mwa
nchi hiyo kwenye miji Temne na Limba wakati chama cha upinzani cha SLPP
chenyewe kina umaarufu mkubwa kusini mwa nchi hiyo hasa kwenye jamii ya Mende.
KINARA WA UPINZANI NCHINI SIERRA LEONE AMTUHUMU RAIS ANAYEMALIZA MUDA WAKE.
Reviewed by safina radio
on
March 26, 2018
Rating:
No comments