SARA MSAFIRI APEWA SIKU 30 KUHAKIKISHA ANATATUA NA KUMALIZA MIGOGOROYA ARDHI.
MANYARA.
Mkuu wa wilaya ya Hanang’ Mkoani
Manyara Bi Sarah Msafiri amepewa siku 30 kuhakikisha kuwa anatatua na kumaliza
migogoro yote ya ardhi iliyopo ndani ya Wilaya yake ambayo imekuwa
ikikwamisha Shughuli za maendeleo.
Agizo hilo lilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Bw Alexander Mnyeti wakati alipokuwa akizungumza na watumishi,na taasisi mbalimbali wilayani Hanang’ ambapo amesema migogogro hiyo baina ya kata na kata,vijiji na vijiji ndio unaowaathiri wananchi hao kwa kutumia muda wao mwingi katika migogoro badala ya kufanya shughuli za maendeleo.

Mkuu wa wilaya ya Hanang’ Mkoani Manyara Bi Sarah Msafiri. |
Bw Mnyeti amesema kuwa kila anayesababisha migogoro ya ardhi anatakiwa
kukamatwa na kuchukuliwa hatua kwani Serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi
pamoja na muda kutatua migogoro hiyo huku wanaosababisha wakiachwa bila
kuchukuliwa hatua za kisheria.
Awali akisoma risala kwa mkuu wa mkoa Mkuu huyo wa Wilaya amesema kwa kipindi cha mwaka 2017/18 kulikuwa na jumla ya migogoro 63 ambapo migogoro mingi imetokea baada ya kuanzishwa kwa vijiji vipya mwaka 2014 lakini mpaka sasa tayari migogoro 18 imeshatatuliwa.
Hata hivyo ametaja sababu zingine
zinazochangia Migogoro hiyo kuwa, ni pamoja na Mihutasari iliyounda vijiji
hivyo kutofautiana na Government Notice yaani GN, Baadhi ya vijiji kuanzishwa
kwa kutumia nyaraka zenye mapungufu ikiwemo mihutasari ya mikutano mikuu, na
baadhi ya wawekezaji wa mashamba makubwa kutokutumia maeneo yote
waliyomilikishwa kisheria.
SARA MSAFIRI APEWA SIKU 30 KUHAKIKISHA ANATATUA NA KUMALIZA MIGOGOROYA ARDHI.
Reviewed by safina radio
on
March 14, 2018
Rating:
No comments