UTAWALA WA BEIJING WATOA ORODHA YA BIDHAA ZITAKAZOONGEZEWA USHURU KWA ASILIMIA 25, KWA BIDHAA ZA MAREKANI.
Nchi ya China imeionya Marekani kuwa haiogopi vita vya kibiashara wakati huu ikitishia kutoza kodi ya zaidi ya dola bilioni 3 kwa bidhaa kutoka nchini Marekani katika kile kinachoonekana kujibu tangazo la rais Donald Trump kutoza kodi dhidi ya bidhaa kutoka China.
![]() |
Rais wa Marekani upande wa bendera ya China (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa China Xi Jin-ping (kulia) upande wa bendera ya Marekani. |
Utawala wa Beijing umetoa orodha ya bidhaa ambazo zitalengwa na kuongezewa ushuru wa hadi kufikia asilimia 25 kuwa ni kuanzia kwenye matunda,na nyama ya nguruwe, licha ya kuwa imeshindwa kuchukua hatua zaidi na kuonesha nia ya kuwa na mazungumzo.
Hatua za hivi karibuni zimeshuhudia masoko ya hisa yakiporomoka wakati huu nchini Marekani,huku ikiituhumu Uchina kwa wizi wa haki miliki pamoja na hatua nyingine ambazo sio za haki dhidi ya makampuni yake, ambapo huenda ikachochea vita vya kibiashara.
Hata hivyo Trump hajachukua mara moja hatua za kuweka ushuru mpya, lakini ndani ya majuma mawili waziri wa biashara wa Marekani anatarajiwa kutangaza bidhaa zilizolengwa kwenye amri hiyo ya rais Trump.
UTAWALA WA BEIJING WATOA ORODHA YA BIDHAA ZITAKAZOONGEZEWA USHURU KWA ASILIMIA 25, KWA BIDHAA ZA MAREKANI.
Reviewed by safina radio
on
March 23, 2018
Rating:
No comments