RAIS WA KOREA KASKAZINI AMEANZA ZIARA YAKE NCHINI CHINA
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un ameanza
ziara yake ya kwanza nje ya nchi tangu ashike madaraka mwaka 2011.
RAIS WA KOREA KASKAZINI KIM JONG UN |
Ulinzi umeimarishwa mjini Beijing kama ambavyo
hutokea wakati viongozi wa China
wanapokutana na viongozi wakuu wa mataifa ya kigeni.
Hatua hii inathibitisha taarifa za awali
zilizotolewa na vyombo vya habari vya Japan kuwa afisa wa ngazi ya juu kutoka
Korea Kaskazini amesafiri kwa treni kwenda China.
Hata hivyo msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya
China ameviambia vyombo vya habari kuwa hakuwa na taarifa iwapo Kim Jong Un
anazuru nchini humo.
Ziara hiyo inakuja kabla ya Kim Jong Un
kukutana na rais wa Korea Kusini Moon Jae-in mwezi ujao na ambayo huenda
yakafuatiwa na mazungumzo kati ya kiongozi huyo wa Korea Kaskazini na rais wa
Marekani Donald Trump yanayolenga kupunguza mivutano iliongezeka tangu Trump
aingie madarakani.
RAIS WA KOREA KASKAZINI AMEANZA ZIARA YAKE NCHINI CHINA
Reviewed by safina radio
on
March 27, 2018
Rating:
No comments