WAKANDARASI WATAKIWA KUNUNUA VIFAA VINAVYOTENGENEZWA NCHINI.
Waziri wa maji na umwagiliaji Mhandisi Isack
Kamwelwe amewataka wakandarasi wanaotekeleza miradi mikubwa kununua vitendea
kazi vinavyozalishwa hapa nchini ikiwemo mabomba ya kusafirisha maji kwa lengo
la kukuza uchumi wa ndani.
Waziri wa maji na umwagiliaji Mhandisi Isack |
Mh Kamwelwe ametoa maagizo hayo wakati akizungumza
na wafanyakazi wa mamlaka ya maji safi na maji taka mkoa wa Dar-es-salaam na
Pwani DAWASA,ambapo ameutaka uongozi wa DAWASA kulisimamia agizo hilo kwa
umakini mkubwa .
Kwa upande wake kaimu mkurugenzi wa DAWASA Romanus
Mwandingo amesema kuwa taratibu za ujenzi wa miradi mipya ya maji taka na maji
safi likiwemo bwawa la kidunda linaendelea vizuri.
Hata hivyo agizo hilo la Mh waziri limekuja siku
chache baada ya rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh John Magufuli
kuagiza kutumika kwa bidhaa zinazozalishwa hapa nchini katika mkutano wa 11 wa
wafanyabiashara kuliko kuagiza bidhaa za nje hali inayosababisha viwanda vya
ndani kufa.
WAKANDARASI WATAKIWA KUNUNUA VIFAA VINAVYOTENGENEZWA NCHINI.
Reviewed by safina radio
on
March 21, 2018
Rating:
No comments