IMEELEZWA KUWA BANDARI YA MTWARA INAKUWA KWA KASI.


Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti Maji na Nishati Zanzibar ZURA Mwalimu Ally Mwalimu, amesema kuwa Bandari ya Mtwara inakuwa kwa kasi na bado ina fursa za uwekezaji .


Image result for PICHA YA BANDARI YA MTWARA
SEHEMU YA BANDARI YA MTWARA


Mwenyekiti huyo amesema hayo mara baada ya kutembelea bandari hiyo kwa ajili ya kuangalia na kujifunza mambo mbali mbali na kuweza kuona namna watakavyoweza kutumia bandari hiyo kusafirisha mafuta na bidhaa nyingine.

Aidha, Bw. Mwalimu amesema kuwa Zanzibar wanataka kutafuta njia rahisi za  kusafirisha mafuta kutoka  bandari za Tanzania ambapo awali walikuwa wakichukua mafuta kutoka bandari ya Dar es salaam lakini kutokana na changamoto za bandari hiyo wameamua kupeleka katika bandari nyingine ikiwemo ya Mtwara.

Kwa upande wake Mratibu wa Sekta ya Maji kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kosmasi Komba amesema kuwa ni jambo la kujivunia kuwa  shughuli zinazofanywa na bandari hiyo kuwa zinagusa watu na kwenda kujifunza.

Hata  hivyo, Bandari ya Mtwara inauwezo wa kusafirisha tani laki nne za mizigo mbali mbali kwa mwaka ambapo hadi kumalizika kwa ujenzi wa Gati mpya  mwezi Aprili mwaka 2019 itakuwa na uwezo wa kusafirisha tani laki sita kwa mwaka.  

IMEELEZWA KUWA BANDARI YA MTWARA INAKUWA KWA KASI. IMEELEZWA KUWA BANDARI YA MTWARA INAKUWA KWA KASI. Reviewed by safina radio on March 27, 2018 Rating: 5

No comments

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.