Imebainika kuwa viapo vya miungu vinavyotoka kwenye madhabahu za koo na familia ni kisababisho kikubwa kinachowafanya vijana kukosa ajira



Imebainika kuwa viapo vya miungu vinavyotoka kwenye madhabahu za koo na familia ni kisababisho kikubwa kinachowafanya vijana kukosa ajira,kutokuolewa au kuoa kwa wakati na wengine kujiingiza kwenye matendo maovu yakiwemo matumizi ya dawa za kulevya.


Image result for PICHA YA MGUU WA MTU


Huduma ya redio safina kesho katika ukumbi wa maombi ulioko Mbauda jijini Arusha kuanzia saa mbili hadi saa sita mchana imekuandalia maombi maalum ya kuvunja viapo vya miungu vinavyotoka kwenye koo na familia ili kukomboa fursa za vijana kwa kukanyaga mafuta kama kitendo cha imani.

Aidha kwa mujibu wa somo hilo viapo vya miungu vinavyotoka kwenye madhabahu vimewafanya vijana wengi kukwama kimaisha hasa kwenye mahusiano,ajira,pamoja na elimu jambo ambalo kanisa jamii na taifa kwa ujumla hawana budi kwenda mbele za  Mungu kwa maombi ili kuvunja viapo hivyo.

Pamoja na hayo maombi yatafanyika kwa vijana wote ili kuwafungua dhidi ya roho ya mauti,magonjwa,mahusiano kuvunjika,ukosefu wa ajira, kukomboa vibali vya karama na vipawa, pamoja na makundi yanayoshikiliwa kwenye vifungo vya ulevi,zinaa na matumizi ya madawa ya kulevya.

Hata hivyo maombi hayo yanayokwenda sambamba na kitendo cha imani cha kukanyaga mafuta yamelenga kufungua fursa mbalimbali za vijana ili wawekwe huru na kutumikia kusudi la Mungu lililowekwa ndani mwao.

Imebainika kuwa viapo vya miungu vinavyotoka kwenye madhabahu za koo na familia ni kisababisho kikubwa kinachowafanya vijana kukosa ajira Imebainika kuwa viapo vya miungu vinavyotoka kwenye madhabahu za koo na familia ni kisababisho kikubwa kinachowafanya vijana kukosa ajira Reviewed by safina radio on March 21, 2018 Rating: 5

No comments

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.