HUDUMA YA REDIO SAFINA KESHO KATIKA UKUMBI WA MAOMBI, IMEANDAA MAOMBI MAALUMU YA KUSHUGHULIKIA ROHO YA UTUMWA INAYOWASABABISHIA WATU KUINGIA KATIKA WIMBI LA MADENI KWENYE JAMII.


ARUSHA.

Imebainishwa kuwa kuna uwezekano mkubwa wa adui kuachilia roho ya madeni kwa watu endapo hawatasimama kikamilifu kumshirikisha Mungu kila jambo wanalolifanya hususan biashara.

Image result for roho ya madeni
Kuingia katika wimbi la madeni kutokana na roho ya madeni inayoachiliwa na adui.
Huduma ya redio safina kesho katika ukumbi wa maombi uliopo mbauda jijini Arusha kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa sita mchana imekuandalia maombi maalumu ya kushughulikia roho ya utumwa inayo wasababisha watu kuingia katika wimbi la madeni kwenye jamii.

Aidha kwa mujibu wa somo hilo roho ya madeni imekuwa ikiwatesa baadhi ya watu Kutokana na kushidwa kulipa madeni hayo kwa wakati hali ambayo imevuruga ndoa pamoja na watu kufisiliwa vitu vyao kama vile nyumba,vyombo vya ndani,mifugo,mashamba pamoja na bidhaa walizonunua hata kama hazitokani na fedha walizokopa.

Vilevile somo hilo limebainisha kuwa licha ya roho ya madeni kusababisha watu kufisiliwa pia imesababisha magonjwa kama vile ugonjwa wa moyo ,kisukari,shinikizo la damu na mara nyingine watu kupoteza maisha kutokana na mshtuko pamoja na msongo wa mawazo.

Hata hivyo kesho watu wataombewa kulingana na mahitaji yao hivyo kila mmoja anashauriwa kuwa na imani pamoja na kujipatanisha na Mungu kwa njia ya maombi ya toba ili Mungu awaze kuwaokoa dhidi ya matatizo hayo yanayowakabili.


HUDUMA YA REDIO SAFINA KESHO KATIKA UKUMBI WA MAOMBI, IMEANDAA MAOMBI MAALUMU YA KUSHUGHULIKIA ROHO YA UTUMWA INAYOWASABABISHIA WATU KUINGIA KATIKA WIMBI LA MADENI KWENYE JAMII. HUDUMA YA REDIO SAFINA KESHO KATIKA UKUMBI WA MAOMBI, IMEANDAA MAOMBI MAALUMU YA KUSHUGHULIKIA ROHO YA UTUMWA INAYOWASABABISHIA WATU KUINGIA KATIKA WIMBI LA MADENI KWENYE JAMII. Reviewed by safina radio on March 14, 2018 Rating: 5

No comments