WAZIRI JAFFO ASEMA LENGO LA RAIS KUANZISHA VIWANDA LIMEFIKIA ASILIMIA 49


Waziri wa nchi ofisi ya rais tawala za mikoa na serikali za mitaa Mh Suleman Jaffo amesema kuwa lengo la rais la kuanzisha viwanda mia moja kwa kila mkoa limefikia asilimia 49 katika kipindi cha miezi mine tangu agizo litolewe na rais John Magufuli.


Image result for PICHA YA JAFFO
WAZIRI SULEMAN JAFFO

Mh Jaffo amesema hayo mjini Dodoma katika kikao kilichowahusisha wakuu wa mikoa makatibu tawala na watendaji waandamizi mikoa kwa ajili ya kuandaa bajeti itakayowasilishwa bungeni wakati wa bunge la bajeti.

Amesema kuwa uanzishwaji wa viwanda hivyo mia moja ulikuwa haujawahi kufanywa na wakuu wa mikoa yeyote katika historia ya nchi hii hivyo wakuu hao wa mikoa watakuwa wa kwanza kuanzisha viwanda hivyo.

Kwa upande wake naibu katibu mkuu TAMISEMI Dr Zainabu Chaula amesema kuwa utekelezwaji wa maagizo ya serikali utafanikiwa endapo viongozi wa mikoa wataenda pamoja katika utendaji kazi.

Naye mwenyekiti wa wakuu wa mikoa hapa nchini Mhandisi Evarest Ndikilo ameomba kufanyika kwa mkutano wa pamoja kati ya wakuu hao wa mikoa na watendaji wa taasisi zinazosimamia masuala ya viwanda.

WAZIRI JAFFO ASEMA LENGO LA RAIS KUANZISHA VIWANDA LIMEFIKIA ASILIMIA 49 WAZIRI JAFFO ASEMA LENGO LA RAIS  KUANZISHA VIWANDA LIMEFIKIA ASILIMIA 49 Reviewed by safina radio on March 21, 2018 Rating: 5

No comments

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.