SIDO MANYARA, YAKUTA NA WAJASIRIAMALI WA VIWANDA VIDOGO VYA KUSINDIKA VYAKULA.


Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo Nchini (SIDO) Mkoani  
Manyara  limekutana na Wajasiriamali wa viwanda vidogo vya kusindika vyakula Mkoani humo  kwa lengo la kuwafundisha  namna bora ya kupata mikopo katika benki ya CRDB kupitia skimu ya SIDO.

 Image result for VYAKULA VILIVYOSINDIKWA.

Meneja wa SIDO Mkoani Manyara Abel Mapunda  amesema kuwa  shughuli za sido ni kuendeleza teknolojia kwa wajasiriamali, kutoa elimu ya ujasiriamali, biashara na masoko pamoja na kuwapatia wajasiriamali mikopo  ili waweze kujienedeleza kiuchumi.

Image result for sido tanzania
Aidha, amesema kuwa SIDO imeingia mkataba na watu wa Benki ya CRDB chini ya skimu ya SIDO ili kuwawezesha wajasiriamali hao kupata mikopo mikubwa ambayo itawawewzesha kuendesha viwanda vyao pamoja na kujiinua kiuchumi.

Naye Meneja Biashara kitengo cha mikopo CRDB Denis Kashasha amesema kuwa wana makubaliano kati yao na SIDO kwaajili ya kuwakopesha wajasiriamali wadogo lakini mpaka sasa hakuna mjasiriamali aliyeweza kupata mkopo huo kutokana na kushindwa kutimiza vigezo.

Kwa upande wao wajasiriamali wamelalamikia masharti magumu yaliyowekwa na benki ya CRDB kupitia Mkopo wa skimu ya SIDO na  kuwasababishia kushindwa  kupata mikopo.


SIDO MANYARA, YAKUTA NA WAJASIRIAMALI WA VIWANDA VIDOGO VYA KUSINDIKA VYAKULA. SIDO MANYARA, YAKUTA NA WAJASIRIAMALI WA VIWANDA VIDOGO VYA KUSINDIKA VYAKULA. Reviewed by safina radio on March 22, 2018 Rating: 5

No comments