MAREKANI YATANGAZA KUWAFUKUZA WANADIPLOMASIA NCHINI HUMO.
Nchi ya Marekani pamoja na mataifa mengine manne kwenye umoja wa
Ulaya wametangaza kuwafukuza kwenye nchi
zao wanadiplomasia wa Urusi baada ya tukio la kupewa sumu jasusi wa Urusi jijini London majuma kadhaa yaliyopita.
Rais wa Marekani Donald Trump kwa upande wake ameagiza kufukuzwa
nchini humo kwa maafisa 60 wanaodaiwa kuwa ni majasusi wa Urusi katika kile
kinachoonekana ni kujibu mapigo kutokana na tukio la kupewa sumu kwa jasusi
wake wa zamani mjini Salisbury.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje Sarah Sanders amesema hatua
hiyo imetokana na juhudi za kidunia dhidi ya Urusi hatua zilizochukuliwa baada
ya Urusi kudaiwa kutumia sumu yenye kemikali kwenye ardhi ya Uingereza.
Marekani inasema maofisa 48 ambao hawajulikani wako Marekani na
wengine 12 kwenye umoja wa Mataifa na sasa wanazo siku 4 kuondoka Nchini
Marekani.
Rais Trump pia ameagiza kufungwa kwa ofisi za ubalozi wa Urusi
mjini Seattle, ofisi ambazo Marekani inasema zilikuwa zinatumiwa na Urusi
kufanya ujasusi.
Katika hatua nyingine mataifa 14 ya umoja wa Ulaya yanawafukuza wanadiplomasia wa
Urusi katika kile kinachoonekana ni kuungana na nchi ya Uingereza dhidi ya
Urusi inayotuhumiwa kutumia sumu dhidi ya jasusi wake wa zamani.
MAREKANI YATANGAZA KUWAFUKUZA WANADIPLOMASIA NCHINI HUMO.
Reviewed by safina radio
on
March 27, 2018
Rating:
No comments