RAIS WA URUSI VLADIMIR PUTIN ANAJIANDAA KUONGOZA TAIFA HILO KWA MIAKA MINGINE SITA


Rais wa Urusi Vladmir Putin anajiandaa kuongoza taifa hilo kwa miaka sita mingine baada ya kupata ushindi wa kishindo katika uchaguzi mkuu wa rais ambao hadi sasa ni washirika wake wa karibu ndio waliompongeza wakati huu uhusiano kati ya nchi yake na mataifa ya magharibi ukisuasua.

Image result for PICHA YA RAIS VLADIMIR PUTIN WA URUSI
RAIS    VLADMIR PUTIN WA URUSI


Rais Putin ambaye ameitawala Urusi kwa karibu miongo miwili, amepata ushindi wake wa kwanza mkubwa wa asilimia 76.67 ya kura zote lakini akakanusha pia taarifa kwamba amepanga kuwa rais wa kudumu.
Upinzani unasema kuwa matokeo hayo yametengenezwa, ukidai kuwa kuna masanduku ambayo kura ziliwekwa kabla, pamoja na matukio mengine ya ukiukwaji wa sheria za uchaguzi.
Awali utawala wa Moscow ulikuwa umehamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye zoezi la upigaji kura katika kile kilichoonekana ni kujaribu kuufanya uchaguzi huo uwe wa kuaminika.
Rais Putin ambaye sasa ataongeza muda wa utawala wake hadi mwaka 2024 tayari ni kiongozi aliyeoongoza taifa hilo kwa muda mrefu zaidi tangu kumalizika kwa utawala wa Stalin.

RAIS WA URUSI VLADIMIR PUTIN ANAJIANDAA KUONGOZA TAIFA HILO KWA MIAKA MINGINE SITA RAIS WA URUSI VLADIMIR PUTIN ANAJIANDAA KUONGOZA TAIFA HILO KWA MIAKA MINGINE SITA Reviewed by safina radio on March 19, 2018 Rating: 5

No comments