WAKULIMA GEITA WATAKIWA KUWA WAANGALIFU KWA MAZAO WANAYOYAPATA PAMOJA NA KUYATUMIA KWA FAIDA.
Wito umetolewa kwa wakulima wa kijiji cha Isamilo,
wilayani Geita mkoani Geita, kuwa waangalifu kwa mazao wanayoyapata pamoja
na kuyatumia kwa faida.
Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Geita Emily Kasagara. |
Wito huo umetolewa na Katibu Tawala Msaidizi Uchumi
na Uzalishaji Mkoa wa Geita Emily Kasagara, wakati wa mavuno ya pamoja ya mahindi ya mbegu ya
mahindi aina ya WEMA 2109 yaliyofanywa
na wakulima wa kijiji cha Isamilo Wilayani Geita, Mkoani Geita.
Mavuno hayo ya pamoja yamefanyika katika moja ya
shamba darasa wilayani Geita ambapo wakulima hao wamesema kuwa mbegu hizo
zinastahimili ukame na kutoa mazao mengi.
Aidha, Wakulima hao wa Kijiji cha Isamilo wamepongeza
mradi wa mbegu hiyo ya mahindi aina ya WEMA 2109 iliyotolewa na Tume ya Taifa
ya Sayansi na Teknolojia COSTEC kwa kushirikiana na Jukwaa la Bio Teknolojia kwa
Maendeleo ya Kilimo-OFAM.
Hata hivyo, Mwaka jana Tume ya Sayansi na
Teknolojia-COSTEC na Jukwaa la Bio Teknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo-OFAM
walitoa mafunzo kwa maafisa ugani na baadae wakaenda kupanda mbegu katika shamba
darasa mbali mbali mkoani Geita.
WAKULIMA GEITA WATAKIWA KUWA WAANGALIFU KWA MAZAO WANAYOYAPATA PAMOJA NA KUYATUMIA KWA FAIDA.
Reviewed by safina radio
on
March 23, 2018
Rating:
No comments