MIKOA YA KASKAZINI MWA TANZANIA YA ATHIRIKA ZAIDI KWA UGONJWA WA FIGO.
DAR-ES-SALAAM.
Utafiti umebaini
kuwa kila watu kumi mmoja anatatizo la figo huku mikoa ya Kaskazini mwa
Tanzania ikionekana kuwa asilimia saba ya wananchi waliofanyiwa utafiti katika
maeneo yao wanatatizo la ugonjwa wa figo hali inayoonyesha tatizo hilo kuwa
kubwa nchini.
![]() |
figo lililoshambuliwa na magonjwa. |
Hayo yamebainishwa
leo na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Figo kutoka Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili jijini Dar es salaam Dk. Onesmo Kisanga ambapo amesema kuwa kina mama
wengi ni waathirika wakubwa wa tatizo hilo la figo kuliko wanaume kutokana na
uzazi.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Figo, Onesmo Kisanga wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) LEO akizungumzia kuhusu umuhimu wa kupima afya mara kwa mara ili kuzuia uwezekano wa mtu kupata matatizo makubwa ya magonjwa ya figo.
Aidha, Dk. Kisanga
amesema kuwa katka maadhimisho ya siku ya figo duniani ambayo huuadhimishwa
kila alhamisi ya pili ya mwezi machi wamelenga zaidi kuwasaidia wakina mama hao
kupata huduma kwa haraka zaidi ili kupunguza tatizo hilo.
Dk. Kisanga amesema
kuwa wakina mama wengi wanakuwa na matatizo mengi wakati wa kujifungua kama
kutokwa na damu nyingi, pamoja na kupata kifafa cha mimba hivyo matatizo hayo
kuweza kupelekea kupata tatizo la figo.
Amesema kuwa
ugonjwa waLupodonor umekuwa unawashambulia zaidi wanawake ambapo kati ya
wanawake ishirini wenyye ugonjwa huo mwanaume mmoja ndiye aliyeathirika.
Hata hivyo,
amebainisha kuwa kwa sasa wameanza kupandikiza figo nchini ambapo mwanzoni mwa
mwezi Novemba mwaka jana madaktari walianza kupandikiza figo ya kwanza katika
hospitali ya Muhimbili sambamba na kuwa serikali imenza kutunga sheria ya
kudhibiti biashara ya figo ambayo itasaidia kuthibiti uuzwaji huo kwa kuwa
anayeuza anamdhulumu anayeuuzia.
MIKOA YA KASKAZINI MWA TANZANIA YA ATHIRIKA ZAIDI KWA UGONJWA WA FIGO.
Reviewed by safina radio
on
March 06, 2018
Rating:

No comments