ZAIDI YA TANI 100 ZA TAKA HUZALISHWA KWA SIKU KATIKA MJI WA TUNDUMA MKOANI SONGWE.
SONGWE.
Wakazi wa Mji wa
Tunduma mkoani Songwe wameanza kukumbwa na hofu ya kupata magonjwa ya mlipuko
kutokana na ongezeko kubwa La taka zinazozalishwa katika mji huo ambapo kwa
siku halmashauri ya mji huo huzalisha tani 150 za taka.
Hayo yabebainika
wakati wa mkutano kati ya wakazi hao na Mkuu wa Wilaya ya Momba Juma Said Rando
uliofanyika katika mji wa Tunduma wametoa kero yao kwa mkuu huyo,ambapo Mkuu
huyo wa Wilaya ameonyesha kukerwa na suala hilo la mrundikano wa taka katika
mji huo wa Tunduma.
Kwa upande wake
Mkuu wa Idara ya Fedha katika halmashauri ya mji wa Tunduma Bw. Onesmo Moga kwa
niaba ya Bwana Afya amekiri kuwa mji wa Tunduma ni mji wenye changamoto ya
mrundikano wa Taka kutokana na Mji huo kutokuwa namiundombinu rafiki na
isiyopitika kwa urahisi.
Hata hivyo Bw. Moga
amewahakikishia wananchi kumaliza kabisa tatizo hilo katika halmashauri ya mji
huo ili kuepusha matatizo mengine yatakayoweza kutokea ya kiafya.
ZAIDI YA TANI 100 ZA TAKA HUZALISHWA KWA SIKU KATIKA MJI WA TUNDUMA MKOANI SONGWE.
Reviewed by safina radio
on
March 06, 2018
Rating:

No comments