URUSI YAPENDEKEZA MKUTANO WA USO KWA USO KWA MAWAZIRI WA MAMBO YA NJE WA PANDE ZOTE.
MOSCOW.
Urusi
imependekeza kuandaliwe mkutano wa ana kwa ana kati ya Waziri wa Mambo ya
Kigeni wa Urusi Sergei Lavrov na mwenzake wa Marekani Rex Tillerson wakati
mawaziri hao wote wakiwa ziarani barani
Afrika.
![]() |
Moscow. |
Naibu
Waziri wa Mambo ya nchi za nje wa Urusi Sergei Ryabkov amesema masuala
yanayostahili kujadiliwa yanaongezeka, ndio maana wametoa pendekezo hilo.
Lavrov
na Tillerson watazuru Ethiopia wiki hii lakini Ryabkov amesema hawana taarifa
yoyote kuhusu kama ratiba zao huenda zikaunganishwa.
Lavrov
alianzia ziara yake ya siku tano barani Afrika jana Jumatatu nchini Angola na
anapanga kuzitembelea Namibia, Msumbiji, Zimbabwe na Ethiopia ambapo atakuwa
katika mji mkuu Addis Ababa mnamo Machi 8 na 9.
Kwa
upande wake Tillerson atazuru nchi za Kiafrika ikiwemo Ethiopia kati ya Machi 6
na 13 kwa mujibu wa msemaji wa wizara ya mambo ya nje.
URUSI YAPENDEKEZA MKUTANO WA USO KWA USO KWA MAWAZIRI WA MAMBO YA NJE WA PANDE ZOTE.
Reviewed by safina radio
on
March 06, 2018
Rating:

No comments