HUDUMA YA REDIO SAFINA KESHO IMEANDAA MAOMBI MAALUM YA KUKAA MBELE ZA MUNGU KWA MUDA MREFU ILI KUOMBA TOBA NA REHEMA JUU YA VITENDO VIOVU.
ARUSHA
Imebainishwa kuwa maadili ya mtu,jamii, au taifa
yanapo poromoka shetani hupata mwanya wa kuingiza roho chafu inayomfanya Mungu
kuachilia adhabu juu ya watu yakiwemo majanga ya njaa na magonjwa.
![]() |
majanga ya njaa. |
![]() |
majanga ya njaa. |
Huduma ya redio safina jijini Arusha kesho kwanzia
saa mbili asubuhi hadi saa sita mchana imeandaa maombi maalumu ya kukaa mbele
za Mungu kwa muda mrefu kwa ajili ya kuomba toba na rehema juu ya vitendo viovu
kama vile unyanyasaji wa kijinsia,wanandoa kuingiliana kinyume na maumbile pamoja
na ndoa za jinsia moja yaani ushoga.
Aidha kutokana na kuporomoka kwa maadili kwa baadi
ya watu katika jamii kumetajwa kuwa chukizo mbele za Mungu na chanzo cha mateso
na kilio katika familia ikiwemo ndoa kuvunjika,kuzidi kwa magojwa ya
zinaa,uchumi kuporomoka kutokana na ghadhabu ya Mungu kuharibu vyanzo vyote vya
uchumi kwa wote wanaoasi sheria na amri zake.
Pia kutokana na laana inayopiga uchumi baada ya kuporomoka kwa maadili kwa
kuwepo na ndoa za jinsia moja ukatili na unyanyasaji kwa wanandoa kesho katika
ukumbi wa maombi uliopo mbauda jijini Arusha kutafanyika maombi ya toba na
rehema kumuomba Mungu aondoe roho chafu ndani ya jamii na kukomboa uchumi wa
mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
HUDUMA YA REDIO SAFINA KESHO IMEANDAA MAOMBI MAALUM YA KUKAA MBELE ZA MUNGU KWA MUDA MREFU ILI KUOMBA TOBA NA REHEMA JUU YA VITENDO VIOVU.
Reviewed by safina radio
on
March 07, 2018
Rating:

No comments