WANAWAKE EAC WAUNGANA NA WANAWAKE WAOTE DUANIA KUADHIMISHA SIKUKUU YAO.


ARUSHA.

Wanawake wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wameungana na wanawake wote duniani kuadhimisha siku ya wanawake kwa kutoa vifaa Tiba katika hosipitali ya mkoa wa Arusha Mt Meru.

Akikabidhi vifaa hivyo Naibu Katibu mkuu  wa Jumuiya  hiyo,Jescah Eriyo amesema kuwa anatambua moyo wa kina mama katika kuifanya  kazi hivyo ambapo amewataka kuendelea kufanya kazi kwa moyo wa kujitoa na kutambua kuwa mwanamke ana nafasi kubwa katika jamii.

Akitoa shukrani  kwa niaba ya wafanyakazi wa hospitali hiyo mganga mfawidhi Dr Jackline Urio ameishukuru jumuiya  hiyo kwa kuona umuhimu wa kutoa vifaa Tiba katika hospitali  hiyo kwani ni jambo lenye tija  katika jamii .

Hata hivyo miongoni mwa vifaa vilivyotolewa ni pamoja na mashuka  huku vifaa  tiba vyenye thamani  ya dola elfu nne vikitarajiwa kukabidhiwa hivi karibuni katika hosipitali hiyo na Jumuiya hiyo.

Naye Naibu Meya wa Jiji la Arusha Viola  Likindikoki amesema kuwa changamoto za wanawake bado zinatajwa hususani maeneo ya vijijini  ikiwemo ukeketaji wa watoto wa kike kwa baadhi ya jamii, mwanamke kunyanyaswa pindi anapotafuta ajira pamoja na wengine kutopata haki zao.



WANAWAKE EAC WAUNGANA NA WANAWAKE WAOTE DUANIA KUADHIMISHA SIKUKUU YAO. WANAWAKE EAC WAUNGANA NA WANAWAKE WAOTE DUANIA KUADHIMISHA SIKUKUU YAO. Reviewed by safina radio on March 08, 2018 Rating: 5

No comments

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.