MNYETI AAHIDI KUWAPELEKA WATAALAMU WA ARDHI KUTOKA DODOMA KWENDA MANYARA .
MANYARA.
Mkuu
wa Mkoa wa Manyara Bw Alexsander Mnyeti ameahidi kuwaleta wataalamu wa Ardhi
kutoka Mkoani Dodoma ili kumaliza mgogoro wa ardhi ulioleta mtafaruku dhidi ya
wananchi wa Kijiji cha Kimotorok Wilayani Simanjiro na Pori tengefu la
Mkungunero.
![]() |
Bw Alexsander Mnyeti. |
Akizungumza
Wilayani Simanjiro katika Ziara yake ya siku moja Bw Mnyeti ametembelea na
kukagua eneo hilo ambalo limekuwa likilalamikiwa na wananchi kwa muda mrefu na
kuahidi kuleta wataalamu ambao watabainisha mipaka halisi ya eneo hilo.
Mkuu
huyo wa Mkoa amewataka wakuu wa mamlaka ya hifadhi kuacha kujiwekea mipaka
kiholela bila kuwashirikisha wananachi na halshashauri badala yake kazi
hiyo ifanywe na Halmashauri kwa kuwa inamamlaka isiyoegemea upande wowote.
Pia
amesema kuwa ili kumaliza migogoro baina ya hifadhi na wananchi,wataomba mipaka
ibadilishwe ili kuwaachia nafasi wananchi waliokuwa wakiishi kwa muda mrefu
katika eneo hilo.
Aidha
baadhi ya Wananchi wa eneo hilo wamesema kuwa zoezi hilo la kusogezwa kwa
mipaka ya hifadhi kwenye maeneo yao yalianza mwaka 2004 ambapo awali
mpaka wao ulikuwa mwisho wa uwanja wa ndege ambao ulichongwa miaka ya 1980 na
wananchi.
Katika
hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Zephania
Chaula kuhakikisha kuwa ndani ya siku nne anatatua mgogoro wa viongozi wa serikali
ya kijiji cha Narokauwo ambao umewasababisha wananchi kuikataa serikali hiyo.
MNYETI AAHIDI KUWAPELEKA WATAALAMU WA ARDHI KUTOKA DODOMA KWENDA MANYARA .
Reviewed by safina radio
on
March 08, 2018
Rating:

No comments