MKUU WA WILAYA YA MONDULI BW. KIMANTA AZITAKA HALMASHAURI NA WADAU KUTENGA MAENEO YA UJENZI WA VIWANDA VIPYA.
ARUSHA.
Mkuu wa Wilaya ya Monduli Bw. Idd Hassan Kimanta amezitaka Halmashauri zote pamoja na wadau kuhakikisha wanatenga maeneo ya ujenzi wa viwanda vipya ili kuweza kuwavutia wawekezaji sambamba na kujenga uchumi wa kati.
Kimanta ameyasema hayo wakati
akifungua Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Mrisho
Gambo kikao kilicholenga kupitia na kuidhinisha mipangp ya bajeti ya
sekretariet ya Mkoa na halmashauri zote kwa mwaka ujao wa fedha 2018/19.
Kimanta amesema kuwa bajeti hiyo
ambayo ilijadiliwa katika ngazi ya Mkoa na kuwasilishwa kwa wajumbe imeonesha
mafanikio kwa mwaka wa bajeti wa 2017/18 pamoja na changamoto zinazopaswa kuboreshwa
katika kipindi cha mwaka wa fedha ujao.
Ameongeza kwa kusisitiza halmashauri
kuendelea kusimamia zoezi la ukusanyaji wa mapato ya ndani kwani mwezi februari
2018 walikusanya mapato ya ndani kwa asilimia 57 huku wakitakiwa kukusanya mapato kwa asilimia 100 ifikapo mwishoni mwa mwezi
June mwaka huu.
Pamoja na hayo amezitaka halmashauri
zijikite katika kukamilisha miradi ya maendeleo yenye kuleta tija kwa wananchi
badala ya kuwa na miradi mingi ambayo haina tija na viongozi wa serikali
kuwahimiza wananchi kujishughulisha na sekta za ufugaji,kilimo,utalii,viwanda
na biashara ili kujiinua kiuchumi.
MKUU WA WILAYA YA MONDULI BW. KIMANTA AZITAKA HALMASHAURI NA WADAU KUTENGA MAENEO YA UJENZI WA VIWANDA VIPYA.
Reviewed by safina radio
on
March 08, 2018
Rating:
No comments