KIHAMIA AWAOMBA WAFADHILI KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KATIKA KUTATUA CHANGAMOTO ZINAZOIKABILI TAASISI ZA KIELIMU.


ARUSHA.

Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Bw Athuman Kihamia amewaomba wafadhili mbalimbali kushirikiana na serikali katika kutatua changamoto mbalimbali zinazokabili baadhi ya shule za msingi hapa nchini ikiwemo miundombinu ya vyoo na madarasa.

Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Bw Athuman Kihamia.
Bw Kihamia ametoa ombi hilo wakati akipokea mradi wa ujenzi wa vyoo vya wanafunzi walemavu wa macho katika shule ya msingi Themi vilivyojengwa na mdau wa elimu Bi Isabela Mwapamba ili viweze kuwasaidia wanafunzi hao ambao bado wanakabiliwa na changamoto kubwa ya miundombinu hasa ya vyoo katika shule wanazosoma.

Amesema kuwa kwa sasa wana uhitaji mkubwa wa matundu ya vyoo kwenye shule za msingi katika jiji la Arusha hivyo amemuomba mfadhili huo kuendelea na upendo wake wa kutatua changamoto hizo kwa kuwashirikisha marafiki  na kumwahidi kuwa serikali itanedelea kushirikiana  nae kwa juhudi zake za kuchangia maendeleo.

Kwa wake bi Isabela Mwampamba ambaye pia ni mmiliki wa shule ya upendo friends amesema kuwa aliamua kujitolea kama mfadhili wa ndani kwa kuwashirikisha marafiki mbali mbali ili kuwezesha kutatua changamoto ya vyoo vya kisasa ambavyo wanafunzi hao  wenye ulemavu wa macho walikuwa wakikabiliwa nayo.

Hata hivyo mradi huo wa vyoo wenye matundu sita umegharimu zaidi ya shilingi milioni 22 hadi kukamilika kwake.



KIHAMIA AWAOMBA WAFADHILI KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KATIKA KUTATUA CHANGAMOTO ZINAZOIKABILI TAASISI ZA KIELIMU. KIHAMIA AWAOMBA WAFADHILI KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KATIKA KUTATUA CHANGAMOTO ZINAZOIKABILI TAASISI ZA KIELIMU. Reviewed by safina radio on March 09, 2018 Rating: 5

No comments

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.