WAKULIMA SIMANJIRO WASHAURIWA KUTUMIA MBOLEA YA KUPANDIA KATIKA MSIMU HUU WA KILIMO ILI KUVUNA MAZAO MENGI.
MANYARA.
Wakulima wa wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara
wametakiwa kutumia mbolea za kupandia mazao katika msimu huu wa kilimo ili waweze
kuvuna mazao mengi na kukuza uchumi wao na kuondokana na umaskini.
Wito huo umetolewa na Afisa Mazao wa halmashauri ya wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara Bw Erick
Shoo wakati akizungumza na Redio Safina kuhusiana na matumizi bora ya mbolea
katika msimu huu wa kilimo wilayani humo.
Amesema kuwa wakulima wengi wa wilaya hiyo hawana
utaratibu wa kutumia mbolea katika kilimo chao kwa madai kuwa ardhi yao ina
rutuba ya kutosha jambo ambalo linawasababishia kuvuna mazao machache na
kuambulia kupata hasara tofauti na matarajio yao.
Aidha Bw Shoo ameongeza kuwa wanaendelea kushirikiana
na watalamu kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa matumizi bora ya
mbolea,ambapo baadhi ya wakulima waliotumia mbolea kwa msimu uliopita wamepata
mafanikio makubwa katika kilimo chao tofauti na wale wanaofanya kilimo cha
mazoea.
Naye mmoja wa mkulima wa halmashauri hiyo kutoka
kijiji cha Langai Bw Daniel Andrea amesema kuwa kinachowafanya wasitumie mbolea
katika kilimo chao ni kutokana na ardhi ya Simanjiro kuwa na rutuba ya kutosha
hivyo wanahofia kuwa kutumia mbolea kunaweza kuwaharibia ardhi yao.
Hata hivyo msimu wa kilimo katika wilaya ya
Simanjiro huanza mwanzoni mwa mwezi March kwa wakulima kuanza kuandaa mashamba
kwa kusafisha kwa kutumia nyenzo mbalimbali ikiwemo Trekta.
WAKULIMA SIMANJIRO WASHAURIWA KUTUMIA MBOLEA YA KUPANDIA KATIKA MSIMU HUU WA KILIMO ILI KUVUNA MAZAO MENGI.
Reviewed by safina radio
on
March 09, 2018
Rating:

No comments