BADRU YAONGEZA IDADI YA WANUFAIKA WA MIKOPO KUTOKANA NA HATUA ZINAZOCHUKULIWA NA BODI HIYO DHIDI YA WADAIWA.
MOROGORO.
Bodi ya Mikopo nchini imeendelea kuongeza idadi ya
wanufaika wa mikopo wanaojiunga na bodi hiyo baada ya hatua mbali mbali zinazoendelea
kuchukuliwa na bodi hiyo dhidi ya wadaiwa wanaochelewa kulipa mikopo.
![]() |
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya mikopo nchini Abdul-Razaq Badru. |
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya mikopo nchini Abdul-Razaq Badru ameseyasema hayo mjini Morogoro wakati wa kikao kazi cha siku mbili kwa maafisa wa madawati ya mikopo kutoka vyuo mbali mbali hapa nchini vinavyopata mikopo.
Aidha, Badru amesema hatua mbali mbali
zilizochukuliwa kwa usimamizi wa sheria iliyopo zimeiwezesha serikali kutoa
mikopo zaidi huku wanafunzi wakiwa wanufaika wakubwa.
Hata hivyo, amesema kuwa kwa mwaka 2018 wanafunzi
laki moja na elfu ishirini na mbli wamepata mikopo kwa bajeti ya shilingi
bilioni 427 iliyotolewa na serikali.
BADRU YAONGEZA IDADI YA WANUFAIKA WA MIKOPO KUTOKANA NA HATUA ZINAZOCHUKULIWA NA BODI HIYO DHIDI YA WADAIWA.
Reviewed by safina radio
on
March 09, 2018
Rating:

No comments