RAIA 24 WAUAWA KUTOKANA NA MASHAMBULIZI MAKALI YA ANGA NA ARDHI, SYRIA.
DAMASCUS.
Mashambulizi makali
ya angani na ardhini yanayoendelea kufanywa na jeshi la Syria katika eneo la
Ghouta Mashariki, limewaua raia 24.
Shirika la haki za
Binaadamu la Syria limethibitisha kuuawa na raia hao katika mashambulizi ya
angani yaliyoendelea hapo jana.
Aidha habari zinaeleza
kuwa jeshi hilo limekaribia kulikamata tena eneo hilo linalodhibitiwa na waasi huku
wakisaidiwa na wanajeshi wa Urusi.
Msafara wa malori ya
misaada ya Umoja wa Mataifa na Shirika la Msalaba Mwekundu uliotarajiwa kwenda
katika eneo hilo jana, ulishindwa kutokana na mashambulizi makali
yanayoendelea.
Zaidi ya raia 930
wameuawa katika mashambulizi hayo ya karibu wiki tatu kwenye ngome hiyo ya
mwisho ya waasi nje ya mji mkuu Damascus, ambako watu kadhaa walishambuliwa na
silaha za sumu.
RAIA 24 WAUAWA KUTOKANA NA MASHAMBULIZI MAKALI YA ANGA NA ARDHI, SYRIA.
Reviewed by safina radio
on
March 09, 2018
Rating:

No comments