IMEBAINISHWA KUWA KUNA UWEZEKANO MKUBWA WA ADUI KUTUMIA MAJINA YA WATU VIBAYA KWA MAENEO AU VITENDO NA KUHARIBU MSINGI WA MAISHA IKIWEMO UCHUMI NA AFYA.
ARUSHA
Imebainishwa kuwa kuna uwezekano mkubwa wa adui
kutumia majina ya watu vibaya kwa maneno au vitendo na kuharibu msingi wa
maisha ikiwemo uchumi na afya.
![]() |
ADUI KUTUMIA VIBAYA JINA. |
Huduma ya redio safina kesho katika ukumbi wa maombi
uliopo mbauda jijini Arusha kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa sita mchana
imekuandalia maombi ya ukombozi wa jina la mtu na majina ya mahali anapoishi ili
kudhibiti malango mabaya ambayo yamefunguliwa na adui kupitia jina.
Aidha kwa mujibu wa somo hilo wapo watu wengi ambao
wanataabika kwa magonjwa sugu,umaskini,kufa kwa miradi,ndoa kuvunjika,pamoja na
huduma,kutokana na baadhi ya majina ya watu hao kubeba roho ya mauti.
Pia wapo wengine ambao majina yao yamepelekwa kwa wachawi
na waganga wa kienyeji kwa lengo la kuondoa uhai au kurudisha nyuma maendeleo
ya watu lakini imebainika kuwa damu ya Yesu Kristo ina uwezo wa kusafisha
majina hayo na mtu kuwekwa huru.
Hata hivyo kesho mahitaji mbalimbali yataombewa
katika ukumbi wa safina redio yakiwemo magonjwa,matatizo ya ajira,migogoro ya
ndoa,pamoja kukomboa malango ya majina yaliyokuwa yakipitisha mauti au uchumi
kuyumba.
![]() |
kukomboa malango ya majina. |
IMEBAINISHWA KUWA KUNA UWEZEKANO MKUBWA WA ADUI KUTUMIA MAJINA YA WATU VIBAYA KWA MAENEO AU VITENDO NA KUHARIBU MSINGI WA MAISHA IKIWEMO UCHUMI NA AFYA.
Reviewed by safina radio
on
March 09, 2018
Rating:

No comments