WATU 16 WAFA KWA RADI NCHINI RWANDA.
TAREHE 12 MARCH 2018
Watu 16 waliouawa Jumamosi iliyopita baada ya kupigwa radi
wakiwa katika Kanisa la Waadventista Wasabato katika Wilaya ya Nyaruguru nchini
Rwanda wamezikwa.
Wauamini wote walizikwa katika Makaburi ya Nyabimata katika
mazishi ambayo yalihudhuriwa na mamia ya waombolezaji.
Meya wa Wilaya ya Nyaruguru Habitegeko Francois ameliambia
Shirika la Habari za Ufaransa AFP kuwa watu 14 walipoteza maisha hapo hapo huku wengine wawili wakipoteza
maisha wakiwa hospitalini.
Waumini wengine 140 walijeruhiwa kutokana na radi hiyo
iliyoambatana na mvua kubwa na wanaendelea kupata matibabu katika hospitali
mbalimbali katika Wilaya hiyo.
Mwanafunzi mmoja alipoteza maisha huku wengine 17 wakijeruhiwa
katika tukio hilo baya la kiasili kuwahi kutokea Rwanda katika siku za hivi
karibuni
WATU 16 WAFA KWA RADI NCHINI RWANDA.
Reviewed by safina radio
on
March 12, 2018
Rating:
No comments