NKURUNZIZA ATEULIWA KIONGOZI WA MAISHA
TAREHE 12 -03-2018
![]() |
RAIS NKURUNZIZA WA BURUNDI. |
Chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD kimemtangaza rais
Pierre Nkurunziza kuwa kiongozi wa juu kabisa wa chama hicho, hatua inayomfanya
awe kiongozi wa maisha.
Licha ya taarifa ya chama hicho iliyotolewa mwishoni mwa juma
kutoeleza kwa kina kuhusu nafasi mpya waliyompa Nkurunziza, lakini ni wazi sasa
kiongozi huyo anafanywa kuwa mtawala wa maisha, hatua inayozidisha sintofahamu
zaidi kwenye siasa za nchi hiyo.
Haijafahamika ikiwa kutakuwa na marekebisho mengine ya katiba
tofauti na yale yanayotarajiwa kupigiwa kura mwezi Mei mwaka huu ambapo ikiwa
yataidhinishwa yatamruhusu kuwania urais kwenye uchaguzi wa mwaka 2020 na
kumfanya abaki madarakani hadi mwaka 2034.
Hali ya kisiasa nchini Burundi imekuwa mashakani tangu mwaka
2015, wakati kiongozi huyo alipoamua kuwania urais kwa muhula wa tatu kinyume
cha mkataba wa amani wa Arusha.
Wapinzani wake walijitokeza kuandamana, hatua ambayo
iliikasirisha serikali ya Bujumbura ambayo ilitumia nguvu dhidi ya waandamanaji
na kusababisha mamia ya watu kupoteza maisha na maelfu kuyakimbia makazi yao.
NKURUNZIZA ATEULIWA KIONGOZI WA MAISHA
Reviewed by safina radio
on
March 12, 2018
Rating:

No comments