MKUU WA WILAYA YA GEITA HERMAN KAPUFI AMEPOKEA MAFUTA YA KUJIPAKA KWA AJILI YA WATOTO NJITI.
Mkuu wa Wilaya ya Geita Bw Herman Kapufi amepokea
msaada wa mafuta ya kujipaka kwa ajili ya watoto njiti waliolazwa katika Hospitali
ya Rufaa ya Mkoa wa Geita.
![]() |
Mkuu wa Wilaya ya Geita Bw Herman Kapufi. |
Bw. Kapufi amepokea msaada huo kutoka kwa Kituo cha
kusaidia watoto Njiti cha Neya Pre-babies chini ya Mkurugenzi wake Happyness
Mabula,ambapo ameshukuru kwa msaada huo wa mafuta.
Amesema kuwa msaada huo uliotolewa na Bi. Mabula si
wa kutoa tumaini kwa watu wenye watoto hao pekee bali kwa yeye pia ambaye mtoto
wake alizaliwa kabla ya wakati miaka mitatu iliyopita.
Kwa upande Muuguzi Kiongozi wa hospitali hiyo
Charugamba Jackson amezungumzia changamoto ya hospitali hiyo kuwa na chumba
kimoja cha kuhifadhia watoto njiti huku kikiwa na uwezo wa kuhifadhi watoto
wanne pekee.
Aidha, amesema kuwa idadi ya watoto wanaozaliwa
kabla ya wakati katika hospitali hiyo kwa mwezi ni watoto njiti thelathini
wakati uwezo wake ni mdogo wa kuhifadhi watoto hao ambapo ameiomba jamii
kujitokeza katika ujenzi wa wodi itakayokuwa na vyumba hivyo.
MKUU WA WILAYA YA GEITA HERMAN KAPUFI AMEPOKEA MAFUTA YA KUJIPAKA KWA AJILI YA WATOTO NJITI.
Reviewed by safina radio
on
March 12, 2018
Rating:

No comments