JUMLA YA WATANZANIA 440,000 WANAKABILIWA NA TATIZO LA SHINIKIZO LA JICHO YAANI GLAUKOMA (GLAUCOMA).
Jumla ya watu laki nne na arobaini wenye umri zaidi
ya miaka 40 na zaidi hapa nchini sawa na asilimia 4.2 wanakabiliwa na tatizo la
shinikizo la macho yaani presha ya macho.
Hayo yameelezwa na mratibu wa huduma za macho mkoa
wa Arusha Dr Mwanahawa Kombo wakati akizungumza na Redio Safina kuhusiana na maadhimisho ya wiki ya shinikizo la ndani ya
jicho yaani Glaukoma inayoadhimishwa duniani kote kuanzia tarehe 11 -17 ya
mwezi Machi kila mwaka.
Dr Kombo amesema kuwa idadi hiyo ya watu ni kwa
mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012,huku chanzo cha tatizo hilo
ikiwa ni mkusanyiko wa magonjwa mbalimbali katika jicho yanayosababisha mnyauko
ndani ya jicho na kumfanya mtu kuwa na uoni hafifu.
Amesema katika maadhimisho ya mwaka huu wao kama
wataalamu wa afya wa mkoa wamejipanga kutoa elimu kwa wananchi ili wafahamu
madhara ya ugonjwa huo kupitia vyombo vya habari ikiwemo Redio,Luninga na
vipeperushi pamoja na kutoa huduma ya upimaji wa macho katika hospitali na
vituo mbalimbali vya afya mkoani Arusha.
Ameongeza kwa dunia nzima kuna watu takribani
milioni mia mbili hamsini na tatu wenye matatizo ya kutokuona vizuri huku kati
ya hao milioni 36 wakiwa hawaoni kabisa.
Hata hivyo kauli mbiu ya maadhimisho ya wiki ya
Glaukoma kwa mwaka huu ni “OKOA UONI WA MACHO YAKO NENDA SASA KAPIME IWAPO UNA
SHINIKIZO LA NDANI YA JICHO’’
JUMLA YA WATANZANIA 440,000 WANAKABILIWA NA TATIZO LA SHINIKIZO LA JICHO YAANI GLAUKOMA (GLAUCOMA).
Reviewed by safina radio
on
March 12, 2018
Rating:
No comments