DK. MWAKYEMBE AWATAKAMAAFISA HABARI NCHINI KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO KWA MUJIBU WA SHERIA, KANUNI, NA TARATIBU ILI KUONESHA WELEDI WA KAZI ZAO.


ARUSHA.
Waziri wa Habari habari, sanaa, utamaduni na michezo Dk.Herson  Mwakyembe amewataka maafisa habari  nchini kutekeleza majukumu yao kwa mujibu  wa sheria, kanuni na utaratibu ili kuonesha weledi wakazi zao.

Akifungua kikao kazi cha 14 cha maafisa habari, mawasiliano na mahusiano, mkoani Arusha leo Dk. Mwakyembe   ametoa maagizo kwa maafisa hao kuwa baada ya mkutano huo unaotarajiwa kudumu kwa siku tano na kumalizika ni wajibu wa kila mshiriki kufanya kazi kwa mujibu  wa sheria ambapo amesema watakaokiuka hatua za kisheria  zitafuatwa.

Aidha, Amesema kuwa wapo maafisa habari  wazembe wasiojishughulisha na kutafuta habari za wizara, taasisi  na kusubiri hadi taasisi itangaze kuwepo kwa mkutano, ziara na mambo kama hayo jambo alilosema ni uzembe na kudhalilisha taaluma huku akiwataka  kwenda na wakati kutoa habari za taasisi,Halmashauri kila Mara ili kuhabarisha umma na serikali kwa ujumla.

Amewataka pia kujenga ushirikiano mzuri baina  yao na vyombo vya habari vilivyo wazunguka ili kuhakikisha taarifa zinafikia umma ambapo amesema siyo kila taarifa ni taarifa ya kutoa bali  zile zilizosahihi ambapo ushirikiano kati ya vyombo vya  habari na Maafisa hao utafanya  kufikisha taarifa sahihi.

Pia, Amezitaka wizara, Halmashauri, pamoja na taasisi  kuwapatia vifaa vya kazi  maafisa habari ili waweze kutekeleza majukumu kwa urahisi ambapo amesema kama wizara au taasisi haziwapatii vifaa  hiyo ni changamoto na taasisi, wizara hizo zitakuwa tatizo.

Naye mwenyekiti wa chama cha maafis mawasiliano serikalini (TAGCO) Pascal Shelutete amesema lengo la  kuanzishwa kwa Chama hicho ni pamoja na kuhakikisha inaendeleza tasnia ya mawasiliano katika weledi unaotakiwa  kwa wanatasnia wote kutoka serikali kuu hadi serikali za mitaa.

Kwa upande wa mwakilishi wa Umoja wa mataifa  Alvaro Rodriguez amesema  Umoja wa mataifa unapenda kuwa washirika wa serikali katika mawasiliano ya maendeleo nchini kwa kuwa nao ni watumishi wa umma.

Hata hivyo kauli mbiu ya mkutano huo wa maafisa habari,mawasiliano,Mahusiano na itifaki ni ' Je Mawasiliano ya kimkakati yanachangiza vipi Tanzania ya viwanda'



DK. MWAKYEMBE AWATAKAMAAFISA HABARI NCHINI KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO KWA MUJIBU WA SHERIA, KANUNI, NA TARATIBU ILI KUONESHA WELEDI WA KAZI ZAO. DK. MWAKYEMBE AWATAKAMAAFISA HABARI NCHINI KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO KWA MUJIBU WA SHERIA, KANUNI, NA TARATIBU ILI KUONESHA WELEDI WA KAZI ZAO. Reviewed by safina radio on March 12, 2018 Rating: 5

No comments

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.