TAKRIBANI WATU MILIONI 253 WANAMATATIZO YA KUTOKUONA VIZURI DUNIANI.


DAR ES SALAAM.

Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto Dk. Phaustin Ndugulile amesema kuwa takwimu zinazotolewa na Shirika la Afya Duniani-WHO zinaonesha kuwa watu takribani milioni 253 duniani wana matatizo ya kutokuona vizuri.

Dk. Ndugulile ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam katika  maadhimisho ya wiki ya kuongeza uelewa kuhusu ugonjwa wa shinikizo la macho duniani.

Naibu Waziri huyo amesema kuwa kutokana na takwimu hizo za WHO watu milioni 36 hawaoni kabisa huku zaidi ya asilimia 75 ya  visababishi vya ugonjwa huo vikiwa vinawezo wa kuzuilika au kutibika kabisa.

Aidha, amesema kuwa takwimu zinaonesha kuwa Tanzania inakadiriwa kuwa asilimia 4.2 sawa na watu laki nne na elfu nne wenye umri zaidi ya miaka arobaini wanakabiliwa na tatizo la shinikizo la macho.

Hata hivyo amesema kuwa asilimia sabini hadi tisini ya watu wenye ugonjwa huo hawafahamu kuwa,kama wanaugua kutokana na kutokuwa na tabia ya uchunguzi wa afya ya jicho kufuatana na ushauri unaotolewa na wataalamu wa afya.


TAKRIBANI WATU MILIONI 253 WANAMATATIZO YA KUTOKUONA VIZURI DUNIANI. TAKRIBANI WATU MILIONI 253 WANAMATATIZO YA KUTOKUONA VIZURI DUNIANI. Reviewed by safina radio on March 12, 2018 Rating: 5

No comments

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.