HUDUMA YA REDIO SAFINA IMEANDAA MAOMBI MAALUMU YA KUVUSHWA MIPAKA KWA MTU PAMOJA NA KUSHUGHULIKIA WACHAWI NA WAGANGA WA KIENYEJI AMBAO WAMEKUWA KIAMBAZA KATIKA MAFANIKIO YA WENGI.
ARUSHA.
Imebainishwa kuwa upo
uwezekano mkubwa wa wachawi na waganga wa kienyeji kukamata ufahamu wa mtu na
kumfanya kushindwa kufanya jambo lolote la msingi kwasababu ya kuwekewa mipaka
kiroho na kimwili kwa njia za ushirikina.
Huduma ya redioa safina
kesho katika ukumbi wa maombi uliopo mbauda jijini Arusha kuanzia saa mbili
asubuhi hadi saa sita na nusu mchana imekuandalia maombi maalumu ya kuvushwa
mipaka ikiwa ni pamoja na kuwashughulikia wachawi na wanganga wa kienyeji ambao
wamekuwa kiambaza katika mafanikio ya wengi.
Aidha wapo baadhi ya
watu ambao wameshindwa kutambua majira na nyakati sahihi za wao kufanya
biashara,kulima,kufuga,kusoma,kuoa au kuolewa kutokana majira na nyakati zao
kukamatwa na wachawi na hatimae kuishia kuwa watu wasiokuwa na makao katika
jamii baada ya adui kuwawekea mipaka.
Kutokana na watu
kuwekewa mipaka pamoja na kukamatwa ufahamu hadi kushindwa kujishughulisha na
kazi yoyote ya kuwapatia kipato baadhi ya watu wamekuwa wavivu,
ombaomba,walevi,wezi,na masikini hali inayowafanya wengi kuwa mzigo katika
jamii na Taifa kwa ujumla.
Hata hivyo kesho katika
ukumbi wa maombi uliopo mbauda jijini Arusha mahitaji mbalimbali yataombewa
sambamba na maombi ya kuwapinga wachawi na waganga wakienyeji ili waweze
kuwaachilia watu waweze kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine kiuchumi na kiroho.
HUDUMA YA REDIO SAFINA IMEANDAA MAOMBI MAALUMU YA KUVUSHWA MIPAKA KWA MTU PAMOJA NA KUSHUGHULIKIA WACHAWI NA WAGANGA WA KIENYEJI AMBAO WAMEKUWA KIAMBAZA KATIKA MAFANIKIO YA WENGI.
Reviewed by safina radio
on
March 12, 2018
Rating:
No comments